Benki CRDB ambao ndio wadhamini wakuu wa Kombe la Shirikisho imesema ilishafanya malipo ya fedha mshindi wa msimu uliopita kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Kauli hiyo ya CRDB imekuja siku moja baada ya Yanga kusema haitocheza mechi ya Fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Singida Black Stars msimu huu hadi itakapolipwa fedha za zawadi za msimu uliopita.
“Tungependa kufahamisha umma na wadau wote wa soka kuwa Benki ya CRDB ni taasisi yenye kuzingatia weledi, kanuni na taratibu na kwa msingi huo tayari Benki ilikwisha tekeleza kikamilifu wajibu wake wa kifedha kwa TFF kama sehemu ya makubaliano ya udhamini wa mashindano haya. Malipo yote ya msimu uliopita yalifanyika kwa TFF kwa mujibu wa mkataba baina ya Benki ya CRDB na TFF,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Jana Jumatatu, Juni 9, 2025, Ałły Kamwe alisema kuwa Yanga inajiandaa kutocheza mechi ya Fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB kwa vile haijapewa fedha zake za zawadi ya ubingwa za msimu uliopita.