You are currently viewing  Samia: Nitanunua matrekta 10,000 kuboresha kilimo

 Samia: Nitanunua matrekta 10,000 kuboresha kilimo

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema atakapochaguliwa kuingoza Tanzania kwa miaka mitano ijayo, Serikali yake itanunua matrekta 10,000 ili kuboresha shughuli za kilimo.

Dkt Samia ameyasema hayo leo, Jumapili Agosti 31, 2025 alipozungumza na wananchi wa Wilaya ya Chemba, mkoani Dodoma, ikiwa ni siku ya pili ya kampeni zake katika Mkoa huo.

“Tuna mpango wa kununua matrekta 10,000 ifikapo mwaka 2030, tuwe tumezinunua hizo na pawatila na zana nyingine za kilimo,” amesema.

Amesema hilo litakwenda sambamba na ununuzi wa zana nyingine, pia kuanzisha vituo katika kanda mbalimbali ambavyo ndani yake pembejeo zote zitapatikana.

Dkt Samia amesema Serikali inalenga kufanya hivyo ili kuwapunguzia wakulima adha ya kwenda kukodi vifaa vya kilimo kwa watu binafsi.

“Bei yoyote mnayolimiwa na watu binafsi, kwa Serikali itakuwa nusu yake,” ameeleza na kuibua shangwe kutoka kwa wananchi waliohudhuria mkutano huo.

Leave a Reply