You are currently viewing Muinjilisti ahukumiwa miaka 30 jela kwa kubaka mtoto wa mwaka 1

Muinjilisti ahukumiwa miaka 30 jela kwa kubaka mtoto wa mwaka 1

Mahakama ya Wilaya ya Pangani, mkoani Tanga, jana tarehe 10 Septemba 2025 imetoa hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela kwa mtuhumiwa Grayson Muze Msemo (miaka 55), baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kubaka mtoto mwenye umri wa mwaka 1 na miezi 4.

Awali, imeelezwa mahakamani kuwa mtuhumiwa ambaye ni muinjilisti na mkazi wa Raskazoni – Tanga, alitenda kosa hilo mnamo tarehe 1 Septemba 2025 katika eneo la Funguni Street, Pangani.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Pangani, Husna Mwiula alisema kuwa mahakama imeridhika na ushahidi uliowasilishwa na kumhukumu mtuhumiwa kifungo cha miaka 30 jela ili iwe fundisho kwa jamii na kuhakikisha haki inatendeka.

Leave a Reply