Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, ameanza rasmi utekelezaji wa vitendo wa mpango wa kupunguza magari katika msafara wake kwa kuhakikisha maofisa wanaofuatana naye wanapanda mabasi, badala ya kutumia magari yao, ili kupunguza matumizi ya mafuta.
Mkuu huyo wa nchi, alitangaza mpango huo alipokuwa jijini Dodoma, Aprili 8, mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya hatua za Serikali na ofisi yake kupunguza matumizi ya mafuta, baada ya vita vinavyoendelea Mashariki ya Kati.
Utekelezaji wa mpango huo, umeshuhudiwa leo, Ijumaa, Aprili 10, 2026 katika msafara wa Dkt Samia uliokuwa na magari machache na basi lililowapakia maofisa waliofuatana naye katika msafara huo.
I
