Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali inalenga kushirikiana na Kenya kuwawezesha vijana katika masuala ya ubunifu na teknolojia.
Amesema hatua hiyo, inalenga kuyafanya mataifa hayo yawe na mnyororo mmoja wa mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) kwa vijana wake.
Dkt Samia ameyasema hayo leo, Jumatatu Mei 4, 2026 alipozungumza na waandishi wa habari, baada ya kikao cha uwili na Rais wa Kenya, William Ruto aliyepo nchini kwa ziara ya siku mbili.
“Isiwe kama sasa hivi, ukiingia kwenye mitandao ya kijamii mheshimiwa Rais alalalalaa… wanatutukana wenyewe na mwisho wana-cross wanatukanana wenyewe kwa wenyewe,” amesema.
