You are currently viewing TAHLISO: Yaliyotokea yasijirudie tena

TAHLISO: Yaliyotokea yasijirudie tena

Rais wa Jumuiya  ya Wanafunzi Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), Geofrey  Kiliba amesema wanavyuo wa mkoa wa Dar es Salaam wanaunga mkono tamko ‘never again’ lililotolewa na vijana Mkoa wa Dodoma mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Kiliba ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Mei 16, 2026 Jumamosi katika kongamano la wanafunzi wa vyuo lenye kauli mbiu ‘never again’ tuipende, tuitunze , tuilinde  nchi yetu’ lililofanyika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam na kuandaliwa na TAHLISO mkoani hapa.

Msingi wa kauli ya Kiliba aliuejenga wakati akieleza madhumuni mahususi ya kongamano hilo huku akirejea ujumbe vijana wa Dodoma waliotoa mbele ya Dkt Samia  kwamba hawako tayari kushirikiana na mtu yeyote anayetaka kuvunja misingi ya amani na mshikamano uliopo huku wakisisitiza yaliyotokea Oktoba 29 yasijirudie tena.