Rais Samia Suluhu Hassan leo ameweka shada la maua katika Kaburi la Mashujaa jijini Moscow Urusi kwa heshima ya wananchi na askari zaidi ya milioni 20 waliopoteza maisha wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.
Rais Samia yuko katika ziara ya kitaifa ya siku tatu nchini Russia ambalo leo mchana anatarajiwa kukutana na mwenyeji wake, Rais Vladimir Putin, katika Ikulu ya Kremlin jijini Moscow.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa kabla ya mkutano huo, viongozi hao wawili wanatarajiwa kuzungumza kwa kina kuhusu masuala anuai yakiwemo biashara, uchumi, uwekezaji na kilimo.
Kesho Rais Samia ataongoza mkutano wa wafanyabiashara wa Tanzania na Russia na pia kuzungumza katika Mkutano wa Kimataifa wa Uchumi utakaofanyika katika jiji la St. Petersburg.
#ZiarayaSamiaUrusi
