You are currently viewing Dkt Samia aifungulia Tanzania milango ya soko la Urusi

Dkt Samia aifungulia Tanzania milango ya soko la Urusi

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amesema hatua ya kuanzishwa kwa safari za moja kwa moja ya ndege za Tanzania kutoka Dar es Salaam hadi Moscow nchini Urusi ni sehemu ya mkakati mpana wa kuimarisha biashara, uwekezaji na utalii kati ya Tanzania na Urusi.

Dkt Samia ametoa kauli hiyo leo, Ijumaa Juni 5, 2026 alipozungumza katika Jukwaa la 29 la Kimataifa la Uchumi la St. Petersburg (SPIEF 2026) nchini Urusi, alikokwenda kwa ziara ya siku mbili ya kikazi.

Amesema Tanzania imeendelea kujijengea sifa duniani kama moja ya vivutio bora vya utalii, huku Serikali ikiweka mazingira yatakayorahisisha watalii na wawekezaji kufika nchini kwa urahisi zaidi.

“Ndege ya kwanza inatajiwa kuanza safari Julai 2, mwaka huu. Tunalenga kuongeza watalii kutoka Urusi hadi kufikia 500,000 kufikia mwaka 2030 na baadaye milioni moja,” amesema.