You are currently viewing Simai: Bajeti ni ya viwango, tujikite kwenye utekelezaji kumsaidia Mhe. Rais

Simai: Bajeti ni ya viwango, tujikite kwenye utekelezaji kumsaidia Mhe. Rais

Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Simai Said, amewataka Watanzania kuelekeza mjadala kwenye utekelezaji wa Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2026/2027, akisisitiza kuwa hicho ndicho kipaumbele kitakachochochea maendeleo na kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Samia katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo ndani ya viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Mhe. Simai alisema mjadala wa sasa unapaswa kujikita katika utekelezaji wa bajeti ili kuhakikisha malengo ya Serikali yanafikiwa kwa manufaa ya Watanzania.

Alipoulizwa kuhusu Yuda ni nani, Mhe. Simai alijibu kwa kifupi, “Nyie ni watu wazima, naamini mmenielewa,” kabla ya kusisitiza kuwa kwa sasa hakuna jambo muhimu zaidi kuliko kuhakikisha Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2026/2027 inatekelezwa kwa ufanisi kwa ajili ya maendeleo ya taifa.