Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imemtunuku Rais Samia Suluhu Hassan tuzo maalum kwa kutambua mchango wake katika kuimarisha mifumo na mazingira ya ukusanyaji wa mapato nchini.
Tuzo hiyo imetolewa leo Julai 1, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa Maadhimisho ya Miaka 30 ya TRA na Utoaji wa Tuzo ya Rais ya Mlipa Kodi Bora.
Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Rais Samia amesema; “Mafanikio haya tusherehekee kwa pamoja na tuzo hii ni ya Watanzania wote.”
Aidha, Rais Samia amesisitiza umuhimu wa walipakodi kulipa kodi kwa hiyari na TRA kuendelea kukusanya mapato bila kutumia mabavu.
Ikumbukwe Julai 2024 Rais Samia aliunda Tume ya Rais ya Kutathmini Maboresho ya Mfumo wa Kodi nchini, hatua ambayo imechangia kuimarika kwa ukusanyaji wa mapato.
