Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar, Mahmoud Mussa Wadi, ameomba wananchi kuwa wasaidizi wa kujenga, kuenzi na kulinda amani na utulivu, pia wadumishe maelewano, kusameheana, kusaidiana na kushirikiana katika kila lenye maslahi kwa Taifa.
Aidha, ameomba viongozi wawe na nguvu ya kufanya maamuzi yenye hekima, yanayoleta watu pamoja, kuondoa mifarakano na kujenga matumaini kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Sheikh Wadi, ameyasema hayo leo, Alhamisi Julai 9, 2026 wakati akisoma dua ya ufunguzi wa hafla ya utiaji saini Tamko la Pmoja la Maridhiano ya Kisiasa visiwani Zanzibar.
