You are currently viewing Tuhuma za ngono zamng’oa Mwendesha Mashtaka Mkuu ICC

Tuhuma za ngono zamng’oa Mwendesha Mashtaka Mkuu ICC

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imemwondoa madarakani Mwendesha Mashtaka Mkuu, Karim Khan kutokana na tuhuma za ukatili wa kingono.

Jana Ijumaa Julai 24,2026 nchi wanachama wa ICC zimepiga kura ya kumwondoa madarakani Khan kutokana na tuhuma hizo. Hata hivyo Khan amekanusha tuhuma hizo.

Uamuzi huo unakuja siku chache baada ya mwanamke aliyetoa tuhuma hizo, anayejitambulisha kwa jina la Sarah pekee, kuzungumza hadharani wakati wa mahojiano na mwanahabari wa CCN Christiane Amanpour.  

Aidha, uamuzi huo umekuja wakati ambao mwenendo wa ICC unaendelea kukosolewa na mataifa mbalimbali likiwemo la Marekani lililosema taasisi hiyo, inavuka mipaka ya mamlaka yake na kutaka ifutwe.

Marekani ilikwenda mbali zaidi ikiweka msimamo wa kutosalimu amri kwa ICC, huku ikiyaomba mataifa mengine kulinda mamlaka yao kitaifa dhidi ya kile ilichodai kuwa tishio la uhuru wa nchi huru.

Rais wa Baraza la Nchi Wanachama wa ICC, Päivi Kaukoranta, amesema nchi wanachama 82 kati ya 125 wa ICC zilipiga kura kuunga mkono kuondolewa kwa Khan.

“Alitenda utovu mkubwa wa nidhamu na kukiuka kwa kiwango kikubwa wajibu wake,” amesema Kaukoranta.