You are currently viewing RC Hamida: Tamasha la Kizimkazi linadumisha muungano wetu
Hamida Mussa Khamis

RC Hamida: Tamasha la Kizimkazi linadumisha muungano wetu

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Hamida Mussa Khamis, amesema Tamasha la Kizimkazi limeendelea kuwa jukwaa muhimu la kuimarisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kuwaleta pamoja wananchi wote.

Akizungumza katika kilele cha tamasha hilo, leo Agosti 14, 2026 katika Uwanja wa Mwehe, Makunduchi, amesema limejenga mazingira ya mwingiliano na fursa za kiuchumi na kuhusisha idadi kubwa ya watu kutoka Tanzania Bara.

Akizungumza kuhusu kaulimbiu ya mwaka huu, ‘Kizimkazi Kumenoga: Shangwe na Fursa’ Hamida amesema sehemu ya shangwe imeonekana kupitia burudani zilizotolewa na wasanii mbalimbali, wakati fursa zikijitokeza kupitia wageni, wafanyabiashara na wadau walioshiriki tamasha hilo.

Amesema uwepo wa idadi kubwa ya watu kutoka Tanzania Bara ni ishara ya tamasha hilo linawaleta Watanzania pamoja na kuimarisha mshikamano na undugu unaojengwa kupitia muungano.