Aliyekuwa Rais wa Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embaló, amehudhuria kilele cha Tamasha la Kizimkazi 2026 visiwani Zanzibar, akiwa mgeni maalum wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Embaló ameshiriki katika hafla ya kilele cha tamasha hilo ambalo limefanyika katika Uwanja wa Mwehe, Makunduchi, na kuwakutanisha wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Tamasha la Kizimkazi 2026, lenye kaulimbiu “Kizimkazi Kumenoga: Shangwe na Fursa,” lilianza Agosti 12 na limefika kilele leo, Agosti 14, 2026, ambapo Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa mgeni rasmi.
