You are currently viewing Watanzania wote kufikishiwa umeme kabla 2030

Watanzania wote kufikishiwa umeme kabla 2030

Rais Samia Suluhu Hassan, amesema dhamira ya Serikali chini ya uongozi wake ni kufikisha umeme Tanzania nzima ifikapo 2030, akidokeza hilo huenda likatokea kabla ya mwaka huo.

Amesema kwa sasa Serikali imepanua wigo wa upatikanaji umeme kwa wananchi kwa kuufikisha katika Vijiji vyote 12,318 na takriban asilimia 62.4 ya vitongoji vya Tanzania Bara.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo, Agosti 22, 2026 alipozungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP), Rufiji mkoani Pwani.

“Dhamira yetu ni kuhakikisha nchi yote inapata umeme ifikapo mwaka 2030 na nadhani tutafikisha lengo hili kabla ya 2030,” amesema.