Rais Samia Suluhu Hassan, amemtaka Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi kuhakikisha anatumia wadhifa aliopewa kukua kiakili badala ya kuharibikiwa.
Mkuu huyo wa nchi, ameyasema hayo leo, Agosti 29, 2026 wakati wa hotuba yake baada ya uapisho wa Ndejembi uliofanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.
Amerejea kauli ya Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, aliyewahi kuwasihi vijana wasiwe kama samaki kwa kadiri anavyokua na akili inaharibika.
Rais Samia, amesema pamoja na kumpa majukumu makubwa, anaamini atayamudu.
