You are currently viewing British Airways kutua Tanzania kutokea London Uingereza

British Airways kutua Tanzania kutokea London Uingereza

Shirika la Ndege la nchini Uingereza, British Airways limetangaza kuanza safari za moja kwa moja kutoka London kwenda Kilimanjaro na Zanzibar nchini Tanzania.

Safari hizo zinazotarajiwa kuanzia Mei 29, 2027, zitafanyika mara tatu kwa wiki kutoka Uwanja wa Ndege wa Gatwick, mjini London, kuelekea Kilimanjaro kisha Zanzibar nchini Tanzania.

Taarifa ya Shirika la British Airways ya leo, Septemba 17, 2026, imeutaja Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kuwa lango la kuelekea baadhi ya maeneo maarufu ya utalii nchini, yakiwamo Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Mlima Kilimanjaro, Ngorongoro, Tarangire na Ziwa Manyara.

Akizungumzia mpango huo, Ofisa Mkuu wa Mipango na Mikakati wa British Airways, Neil Chernoff, amesema shirika hilo limefurahishwa na kuanzisha safari za Kilimanjaro na Zanzibar.

Amesema safari hizo zitaimarisha mtandao wa shirika hilo Afrika Mashariki na kuwawezesha wateja kufikia maeneo mbalimbali ya Tanzania.