Washiriki kutoka nchi mbalimbali duniani wakitoa salamu katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) kuelekea Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), unaotarajiwa kuanza kesho, Oktoba 5, 2026.
Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 2,000 kutoka mabunge 183 wanachama wa IPU, wakiwemo Maspika, Wabunge, Makatibu wa Mabunge na maafisa mbalimbali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kufungua mkutano huo, wenye kaulimbiu: “Kuimarisha Utawala Bora na Kuziwezesha Jamii kupitia Ushirikishwaji, Imani na Fursa kwa Wote.”
