You are currently viewing IPU yamtaja Rais Samia kiongozi wa mfano kwa wanawake

IPU yamtaja Rais Samia kiongozi wa mfano kwa wanawake

Rais wa Wabunge Wanawake wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Cynthia Lopez, amemtaja Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwa mfano wa uongozi wa wanawake duniani, akisisitiza umuhimu wa wanawake kushika nafasi za juu za uongozi na maamuzi.

Lopez amesema hayo leo, Oktoba 5, 2026, wakati akizungumza katika Mkutano wa 153 wa IPU unaofanyika jijini Arusha, akieleza kuwa kuongezeka kwa wanawake katika mabunge kunapaswa kwenda sambamba na kuongezeka kwa ushawishi na nguvu yao katika michakato ya maamuzi.

Amesema hatua hiyo inaonekana kupitia wanawake kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya mabunge, ikiwemo kuongoza kamati, kuwa maspika na kushika nafasi nyingine za juu za maamuzi.

“Tunapokuwa na wanawake wengi zaidi katika mabunge, tunakuwa na ushawishi na nguvu zaidi. Tuna wanawake wanaoongoza kamati, tuna maspika wanawake na tuna viongozi wanawake, kama Rais wa Tanzania, Rais Samia,” amesema Lopez.