Tanzania imeacha kumbukumbu za pekee kwa wajumbe wa Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), waliosema wamevutiwa na ukarimu wa Watanzania, uzuri wa nchi na mapokezi waliyopata.
Waziri wa masuala ya Amani wa Nepal, Ek Nath Dhakal, amesema siku nne walizokaa Tanzania zimewafanya kuipenda nchi hiyo kutokana na uzuri wa watu na ukarimu wao.
Wajumbe wengine, akiwamo Yash kutoka Israel, Dk Sasmit Patra wa India na Les Govender wa Afrika Kusini, wameeleza kufurahishwa na mapokezi mazuri, uchangamfu na upendo walioupata kutoka kwa Watanzania.
Mbali na ukarimu, Dk Vindhya Persaud kutoka Guyana, amesema safari ya kwenda Ngorongoro ilikuwa miongoni mwa kumbukumbu zake bora, baada ya kuwaona wanyama wanne kati ya watano wakubwa maarufu kama Big Five.
#IPU153Tanzania
