Rais Samia azindua majengo, miundombinu ya kisasa Mji wa Serikali Dodoma
Rais Samia Suluhu Hassan, leo Oktoba 30, 2026, amezindua rasmi majengo ya ofisi za Wizara na Taasisi za Serikali pamoja na miundombinu mbalimbali katika Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma, akiwa ameambatana na mgeni maalum Rais wa Angola, Joao Manuel Lourenco.
Rais Samia amezindua majengo ya Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora kwa niaba ya ofisi nyingine zaidi ya 20 zilizopo katika Mji wa Serikali Mtumba.
Uzinduzi huo unalenga kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi, kurahisisha utendaji wa Serikali na kuongeza ufanisi katika shughuli za kiutawala kupitia uwepo wa ofisi za Serikali katika eneo moja lenye miundombinu ya kisasa zaidi.
