Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei mpya za mafuta kwa mwezi Novemba 2026, ambapo kwa Dare es Salaam Petroli itauzwa Shilingi 4,083 kutoka shilingi 4057 sawa na ongezeko la asilimia 0.64.
Kwa upande wa mafuta ya Dizeli yamepanda kwa asilimia 1.03, ambapo kwa sasa yatauzwa 4,128 kutoka 4,086 huku mafuta ya Taa yakiuzwa 4,117 kutoka 4,067 mwezi uliopita.
Mabadiliko hayo ya bei ya mafuta, yataanza rasmi kutumika kuanzia Saa sita usiku kuamkia tarehe 4 Novemba 2026.
Kupanda kwa bidhaa hiyo ya mafuta kwa nchi nyingi duniani kwa sasa, ni kumesababishwa na mgogoro na vita mashariki ya kati, kati ya Israel, Marekani dhidi ya Irani kuliko sababishwa kufingwa kwa malango mkuu wa Hormuz.
Ukiachana na Tanzania, kwa upande wa nchi jirani kwa sasa Kenya mafuta ya petroli kuuzwa 4,607 ikipanda kwa asilimia 6.04 kwa mwezi Oktoba licha kutotangaza bei mpya mpaka sasa, Rwanda Sh 5,228, Zambia Sh 4,377 na Uganda Sh 4,129.
Kwa upande wa dizeli, ulinganisho wa bei za nchi jirani unaonyesha kuwa Kenya inauza kwa takribani Sh 4,622 kwa lita, Rwanda Sh 5,208, Zambia Sh 4,488 na Uganda Sh 4,037, ikilinganishwa na Sh 4,128 za Tanzania, huku utofauti ukiwa kwenye gharama za kuagiza na kusafirisha mafuta, kodi, thamani ya fedha na utaratibu wa kupanga bei unaotumika katika kila nchi.
