You are currently viewing Tanzania kuimarisha ajenda ya nishati safi kupitia COP 31

Tanzania kuimarisha ajenda ya nishati safi kupitia COP 31

Tanzania inatumia jukwaa la Mkutano wa 31 wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31) unaofanyika Antalya, Uturuki, kuimarisha ushirikiano na wadau wa kimataifa katika kufanikisha lengo la kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.

Waziri wa Nishati, Juma Homera, amesema kupitia mkutano huo Tanzania imekutana na wadau mbalimbali walioonesha utayari wa kushirikiana na nchi katika kufanikisha azma hiyo, akiwemo taasisi ya Sustainable Energy for All, ili kuimarisha upatikanaji na matumizi ya nishati safi ya kupikia kuanzia vijijini hadi mijini.

Amesema ushirikiano huo utaongeza nguvu katika utekelezaji wa ajenda ya nishati safi ya kupikia inayohamasishwa na Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye ni kinara wa Umoja wa Afrika (AU) katika kuendeleza matumizi ya nishati safi ya kupikia barani Afrika. #TanzaniaCOP31