You are currently viewing Dkt Samia ataka vitendo kukabili mabadiliko tabianchi

Dkt Samia ataka vitendo kukabili mabadiliko tabianchi

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametaka Mkutano wa 31 wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP31) kuelekeza nguvu katika utekelezaji wa ahadi zilizotolewa badala ya kuishia kwenye matamko, akisisitiza umuhimu wa kufikia matokeo yanayopimika.

Amesema athari za mabadiliko ya tabianchi zinazoikabili Tanzania, zikiwemo ukame, mvua zisizotabirika na kuongezeka kwa kina cha bahari, zinakadiriwa kuigharimu nchi kati ya asilimia mbili hadi tatu ya Pato la Taifa (GDP) kila mwaka.

Ili kukabiliana na hali hiyo, amesema Tanzania na nchi nyingine zinazoendelea zinahitaji kuongezewa fedha za misaada na mikopo yenye masharti nafuu, pamoja na uhamishaji wa teknolojia na kujengewa uwezo.

Ametoa kauli hiyo leo, Novemba 11, 2026, alipohutubia Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali katika Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP31).

#COP31Tanzania