You are currently viewing Watu bilioni moja Afrika hawana nishati safi ya kupikia

Watu bilioni moja Afrika hawana nishati safi ya kupikia

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema takribani watu bilioni moja barani Afrika hawana upatikanaji wa nishati safi ya kupikia, hali inayohitaji juhudi za pamoja za Serikali, sekta binafsi na wadau wa maendeleo kuharakisha upatikanaji wa huduma hiyo.

Akizungumza leo Novemba 12, 2026 katika Mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu Nishati Safi ya Kupikia Barani Afrika, pembezoni mwa Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31), Antalya, Uturuki, Rais Samia amesema changamoto hiyo inahitaji uwekezaji na ushirikiano wa wadau mbalimbali ili kuhakikisha wananchi wanapata nishati salama na nafuu.

“Nishati safi ya kupikia ni muhimu katika kulinda afya za wananchi, kuhifadhi mazingira na kuboresha maisha ya watu wetu. Tunapaswa kuongeza juhudi na uwekezaji ili kuhakikisha hakuna mwananchi anayeachwa nyuma katika upatikanaji wa huduma hii,” amesema Rais Samia. #TanzaniaCOP31