Meli ya MV Mwanza imepoteza mwelekeo na kugonga miamba ya Bismarck wakati nahodha akifanya jitihada za kuitia nanga katika Bandari ya Mwanza, Ziwa Victoria.
Hakuna taarifa zilizoripotiwa kuhusu watu kujeruhiwa kutokana na tukio hilo.
MV Mwanza ni miongoni mwa miradi mikubwa ya serikali katika kuboresha usafiri wa majini nchini Tanzania, ilizinduliwa Januari, 2026
Meli hiyo yenye urefu wa mita 92.6, upana wa mita 17 na ghorofa nne, ilijengwa kwa gharama ya zaidi ya Shilingi bilioni 120 kwa ushirikiano kati ya kampuni za Korea Kusini na taasisi za Tanzania.
Ina uwezo wa kubeba abiria 1,200, tani 400 za mizigo, magari madogo 20 na malori matatu kwa safari moja. Pia ina vifaa vya kisasa vya usalama na mawasiliano vinavyowezesha kutoa taarifa kwa vituo vya utafutaji na uokoaji.
