You are currently viewing Samia: Katiba Mpya itapatikana mwaka 2028

Samia: Katiba Mpya itapatikana mwaka 2028

Rais Samia Suluhu Hassan, amewaambia Watanzania kuwa hivi karibuni ataunda Tume ya Maridhiano, akieleza kuwa mchakato unakwenda vizuri ikiwemo kuwapata wajumbe watakajumuishwa katika tume hiyo.

Ameeleza hayo leo Ijumaa Novemba 20,2026 katika mkutano mkuu wa mwaka wa maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi katika Shule ya Polisi, Moshi (CCP) Mkoa wa Kilimanjaro.

Rais Samia amefafanua kuwa kuitangaza Tume hiyo, atakutana na makundi mbalimbali ya viongozi wa dini na wanasiasa ili kuangalia namna ya kuliendea jambo hilo.

“Hatua iliyofikia ni kuwaandikia barua masharika ya dini ili kupeleka majina yatakayoingia ndani ya Tume. Upande wa vyama vya siasa, taasis za kiraia nadhani tupo vizuri, karibu tutatangaza Tume ya Maridhiano,” amesema Samia.

Rais Samia amesisitiza kuwa kama ambavyo Chama cha Mapinduzi (CCM), kilivyoahidi katika ilani ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, kuwa ifikapo mwaka 2028 na 2029 Katiba mpya itapatikana.