You are currently viewing M-Mama Imesafirisha Wagonjwa Zaidi ya 250,000 Wenye Changamoto za Uzazi-Samia

M-Mama Imesafirisha Wagonjwa Zaidi ya 250,000 Wenye Changamoto za Uzazi-Samia

Rais Samia Suluhu Hassan, Kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama Kupitia Mfumo wa Rufaa wa Kieletroniki wa M-Mama umesaidia kusafirisha wagonjwa zaidi ya 250,000 wenye changamoto mbalimbali za uzazi.

Rais Samia ameyasema hayo leo, Novemba 26, 2026, jijini Dar es Salaam, wakati akifungua Mkutano wa Tatu wa Kisayansi wa Afya.

“Mifumo ya rufaa ikiwemo M-Mama imeunganisha jamii na huduma za dharura za afya ambapo hadi kufikia Agosti, mwaka huu mfumo wa M-Mama umesaidia kusafirisha wagonjwa zaidi ya 250,000, wengine wao wakiwa akina mama na watoto wachanga,” amesema.

Ameongeza kuwa kupitia kampeni hiyo, Serikali imeendelea kuimarisha uwajibikaji kwa kuweka afya ya mama na mtoto kuwa sehemu ya ajenda za viongozi wa mikoa, sambamba na kuboresha huduma za afya na kuhamasisha ushiriki wa jamii katika kulinda afya ya mama na mtoto.