You are currently viewing Aliyetunga jina la Tanzania afariki dunia

Aliyetunga jina la Tanzania afariki dunia

Mtu aliyetunga jina la taifa la Tanzania, Mohamed Iqbal Dar, amefariki dunia akiwa usingizini jijini Birmingham, Uingereza alikokuwa akiishi.

Iqbal alishiriki katika shindano la kutafuta jina la Tanzania lililoandaliwa mwaka 1964 kabla ya muungano ambako yeye alikuwa mmoja wa wanafunzi 80 walioshindana na hatimaye yeye kuibuka mshindi.

Wakati huo Iqbal alikuwa na umri wa miaka 18 na alipewa zawadi ya shilingi 200 za wakati huo.

Leave a Reply