You are currently viewing Boti za bilioni 2 kuboresha afya Visiwani Zanzibar

Boti za bilioni 2 kuboresha afya Visiwani Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amezindua boti tatu za zilizotengenezwa na Kampuni ya QIRO GROUP LIMITED kwa thamani ya Shilingi bilioni mbili. 

Akizungumza katika uzinduzi wa boti hizo za kubeba wagonjwa wakati wa dharura katika Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi, Rais Dk. Mwinyiamesema Serikali imedhamiria kumaliza changamoto za sekta ya afya zinazowakabili wananchi wanaoishi katika visiwa vidogovidogo.

Amefahamisha kuwa boti hizo ni sehemu ya uimarishaji wa huduma za dharura na mfumo wa wa Rufaa kwa Wagonjwa wanaotoka kwenye Visiwa wanaopewa rufaa kutoka vituo vya afya kwenda Hospitali za Wilaya, Mkoa na Taifa.

Rais Dkt. Mwinyi  ameeleza kuwa Serikali imeamua kuzipeleka boti hizo katika maeneo yenye changamoto kubwa zaidi na kwengine  kutafanyiwa utaratibu wa haraka baadae.

Aidha, Dkt. Mwinyi ameishukuru Benki ya Dunia kwa kusaidia gharama za  Ununuzi wa boti tano ambazo tatu tayari zimekamilika na mbili zitakamilika muda mfupi ujao.

Naye Waziri wa Afya, Nassor Ahmed Mazrui  amewahakikishia Wananchi wanaoishi katika  Visiwa  huduma za ihakika zitakazoanza hivi karibuni na kuwa tayari  kuzitumia huduma hizo hususan akina Mama na watoto.

Leave a Reply