You are currently viewing Butiku: Dkt Samia ndiye Rais, tukubaliane na uhalisia Watanzania

Butiku: Dkt Samia ndiye Rais, tukubaliane na uhalisia Watanzania

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere (MNF) Joseph Butiku amewataka Watanzania kukubaliana na uhalisia kuwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ndiye kiongozi wa Taifa hili.

Mzee Butiku mbali na hilo, amesema Rais Dkt Samia amesaidia kuunda Tume ya Kuchunguza Matukio yaliyotokea Oktoba 29, 2025.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Machi 4,2026 wakati wa maadhimisho ya siku ya maridhiano (maridhiano day) yaliyofanyika jijini Mwanza yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Mariadhiano na Amani Tanzania (JMAT).

“Oktoba tulipata tatizo, lakini nataka kuliambia Taifa hili tukubali tunaye Rais wa Jamhuri, hatuna marais 10, tunaye rais mmoja (Rais Samia Suluhu Hassan) ambaye ametuundia Tume itusaidie kujua yaliyotokea tukubali,” na kuongeza kuwa.

“Nimesikia Tume imeomba kuongezewa muda hadi Aprili, tukubali tusubiri aje kutuambia jambo litakalotusaidia katika mazungumzo (maridhiano),” amesisitiza Mzee Butiku.

Leave a Reply