Kamati ya Rufaa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) jana Jumanne, Machi 17, 2026 kwamba, kwa mujibu wa Kifungu cha 84 cha Kanuni za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), Timu ya Taifa ya Senegal imepoteza mechi ya fainali ya fainali hizo iliyochezwa Januari 18, 2026 na matokeo ya mechi hiyo kuwa ushindi wa mabao 3–0 kwa Morocco.
Uamuzi huo unafuatia rufaa iliyowasilishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Morocco (FRMF) kuhusu utekelezaji wa vifungu vya 82 na 84 vya Kanuni za AFCON.
Kamati ya Rufaa ya CAF imetoa majibu na ufafanuzi wa baadhi ya hoja za rufaa hiyo. Rufaa iliyowasilishwa na FRMF imekubalika kisheria na uamuzi wa Kamati ya Nidhamu ya CAF umebatilishwa.
Kamati ya Rufaa ya CAF pia imebaini kuwa mwenendo wa timu ya Senegal unaangukia ndani ya wigo wa vifungu vya 82 na 84 vya Kanuni za AFCON.
Pingamizi lililowasilishwa na FRMF limekubaliwa. Imetangazwa kuwa Senegal (FSF), imekiuka Kifungu cha 82 cha Kanuni za AFCON.
