You are currently viewing DAR yatakiwa kujenga ghorofa kutoa huduma za afya

DAR yatakiwa kujenga ghorofa kutoa huduma za afya

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii katika Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Rashid Mfaume amesema kutokana na uhaba wa maeneo jijini Dar es Salaam ni  vyema  halmashauri zifikirie kujenga majengo ya kutoa huduma za afya kwa muundo wa  ghorofa.

Dkt. Mfaume amesema hayo alipotembelea kituo cha afya cha Kinondoni kwenye ziara yake ya kukagua upatikanaji wa huduma za afya, lishe na ustawi wa jamii katika manispaa ya  Kinondoni, mkoani Dar es salaam.

Aidha, Dkt. Mfaume amevielekeza vituo vya afya vyenye mapato makubwa yatokanayo na wananchi kuchangia huduma kutumia mapato hayo katika kutekeleza miradi mbalimbali ili kufanikisha utoaji wa huduma bora kwa  wananchi ikiwemo ununuzi wa vifaa tiba.

“Niwapongeze kituo cha afya cha Bunju kwa kutumia fedha za mapato ya ndani zaidi ya milioni 172 kununua vifaa tiba. Nivielekeze vituo vyenye mapato makubwa pia kuiga mfano huu wa kituo cha afya cha Bunju” amesisitiza.

Ameongeza kuwa katika kuelekea utekelezaji wa huduma ya bima ya afya kwa wote ni lazima vituo vyote vya afya kuwa tayari kwa ajili ya kuwahudumia wanachama hao kwa huduma mbalimbali.

Leave a Reply