You are currently viewing Daraja la JPM lazidi kufungua fursa za kiuchumi, kijamii

Daraja la JPM lazidi kufungua fursa za kiuchumi, kijamii

Tangu lifunguliwe Juni 19, 2025, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Daraja la JPM (Kigongo–Busisi) lenye urefu wa kilomita 3.0 limeleta mageuzi makubwa ya kiuchumi na kijamii ukanda wa Ziwa Victoria. 

Ujenzi wa daraja hili refu zaidi Afrika Mashariki uligharimu Shilingi Bilioni 610, uwekezaji ambao sasa unadhihirisha thamani yake halisi baada ya mwaka mmoja na nusu wa uendeshaji thabiti.

Ndani ya kipindi hiki, daraja limetokomeza ucheleweshaji kwa kupunguza muda wa kuvuka kutoka saa 2 zilizokuwa zikitumika kwa vivuko hadi dakika 3 hadi 4 tu kwa gari. 

Hatua hii imesisimua ushoroba wa kiuchumi kati ya Mwanza na na mikoa ya kanda ya ziwa, huku ikirahisisha biashara kuelekea Uganda, Rwanda, na Burundi na kugeuza maeneo ya Kigongo na Busisi kuwa korido kuu za kibiashara zinazochochea uchumi wa taifa.