You are currently viewing Dkt Samia: Asiyeendana na kasi yangu atatupisha

Dkt Samia: Asiyeendana na kasi yangu atatupisha

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amesema atachukua hatua za kumuondoa mtendaji yeyote kati ya wateule wake atakayeshindwa kuendana na kasi ya utendaji wake.

Dkt Samia ameeleza hayo leo, Jumatatu Februari 9, 2026 alipozungumza katika hafla ya kuwaapisha wateule wake, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

“Mimi kwangu ni jicho, nani anacheza vipi, nikiona steps zako haziendani na ngoma ninayoipiga, basi utatupisha pembeni niangalie nani mwengine miguu yake mepesi ambaye anaweza akaendana na steps za ngoma ninayoipiga,” amesema. Ametumia jukwaa hilo pia, kufafanua awamu yake hii ya uongozi haitahusisha mabadiliko makubwa ya viongozi, badala yake yatafanyika madogo iwapo atatokea aliyestaafu au asiyeendana na kasi yake.

Leave a Reply