You are currently viewing Dkt Samia awataja mawinga akizindua Soko Kariakoo

Dkt Samia awataja mawinga akizindua Soko Kariakoo

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amesema anatambua juhudi za wafanyabiashara wadogo yaani machinga na mawinga katika kujitafutia kipato, ndiyo maana Serikali yake imejikita katika juhudi za kurasimisha biashara zao.

Dkt Samia ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam leo, Jumapili Februari 8, 2026 alipofungua Soko la Kariakoo lililojengwa upya baada ya kuungua mwaka 2021.

“Natambua juhudi zenu za kujitafutia kipato ndio maana kipaumbele cha Serikali ni kurasimisha biashara zenu kama ilivyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025/30,” amesema.

Leave a Reply