You are currently viewing Dkt. Samia awateua Dk Mpango, Majaliwa kumshauri

Dkt. Samia awateua Dk Mpango, Majaliwa kumshauri

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kumteua Makamu wa Rais mstaafu, Dkt Philip Mpango kuwa mshauri wake wa masuala ya uchumi na miradi.

Pamoja naye, ametangaza kumemteua Waziri Mkuu mstaafu, Kassim Majaliwa kuwa mshauri wake wa masuala ya jamii.

Hata hivyo, uteuzi wa wawili hao ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Dkt Samia wakati wa kampeni za uchaguzi, aliposema ataendelea kuwatumia wawili hao kwa shughuli za Serikali.

Dkt Samia ametangaza uteuzi huo, leo Jumamosi Januari 10, 2026 wakati wa hafla ya kuwapongeza wanamichezo waliofanya vizuri katika mashindano ya kimataifa Ikulu ya Dar es Salaam.

Amesema katikati ya Dkt Mpango na Majaliwa watakaomshauri kwenye masuala ya uchumi, miradi na jamii, kutakuwa na Profesa Palamagamba Kabudi akisema ndiye atakayefanya kazi nao kwa karibu.

“Vile vichwa viwili vikubwa (Dk Mpango na Majaliwa) vinahitaji mtu aliyetulia anayeweza kudili nao. Hawa watoto wangu mara wanaweza kujijibia ikaja kesi, lakini Profesa (Kabudi) anaweza kwenda nao vizuri sana,” amesema.

Leave a Reply