You are currently viewing Dkt Samia awavuta wawekezaji wa sekta ya madini kutoka Urusi

Dkt Samia awavuta wawekezaji wa sekta ya madini kutoka Urusi

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania imebarikiwa kuwa na utajiri mkubwa wa madini muhimu duniani, yakiwemo Uranium, Nickel, Graphite, Helium na madini adimu yanayohitajika katika mapinduzi ya teknolojia na nishati.

Dkt Samia ametoa kauli hiyo leo, Ijumaa Juni 5, 2026 alipozungumza katika Jukwaa la 29 la Kimataifa la Uchumi la St. Petersburg (SPIEF 2026) nchini Urusi, alikokwenda kwa ziara ya siku mbili ya kikazi.

Amesema lengo la Serikali si kuendelea kuuza malighafi pekee, bali kujenga viwanda vya kuongeza thamani ili wananchi wanufaike zaidi kupitia ajira, mapato na ukuaji wa uchumi wa viwanda.

“Tunalenga kuondoka kuwa wazalishaji wa malighafi kuwa wazalishaji wa bidhaa iliyokamilika. Tunawakaribisha washirika kuwekeza nasi katika maeneo ya viwanda ambayo yatatoa tafsiri halisi ya faida ya madini,” amesema.

Jukwaa hilo limewakutanisha zaidi ya washiriki 24,000 kutoka zaidi ya nchi 140, wakiwemo wakuu wa nchi, wawekezaji na viongozi wa makampuni makubwa duniani.