Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan amesema uchaguzi wa mwaka 2025 ulikuwa na mafanikio makubwa ikiwamo kufikia asilimia 44 ya wabunge wanawake huku mchakato huo ukigharamiwa kwa fedha za ndani.

Hata hivyo, licha ya mafanikio hayo, Dkt Samia amebainisha changamoto illyojitokeza ya kuzimwa mtandao na kuwapa pole mabalozi kutokana na usumbufu uliojitokeza, akiahidi kujidhatiti kuikabili hali hiyo isijiridie.
Dkt Samia ameeleza hayo Alhamisi Januari 15,2026 wakati akifungua mwaka wa mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania, hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.
“Washirika wetu jumuiya ya kimataifa na wageni wanaoishi hapa Tanzania, ninatoa pole kwa sintofahamu iliyotokea, kukosekana kwa huduma na kuzimwa kwa mtandao mlikopitia. Ninawahakikishia tumejizatiti kulinda usalama wenu na kuhakikisha hili halitajirudia tena” amesema Dkt Samia.
Kwa mujibu wa Dk Samia, wanatambua kwa moyo mgumu yaliyotokea siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi. Amesema ilikuwa ni muhimu kuingilia kati ili kuilinda amani na usalama kwa mujibu wa Katiba.
“Demokrasia ni safari ya ukuaji na kila safari ya aina hiyo ina maumivu yake, hivyo ni wazi kwamba hivyo ni wazi kwamba hakuna kanuni moja ulimwenguni kwa changamoto hii ya kipekee,” ameeleza.
