You are currently viewing Dkt. Samia: Kilichofanyika leo kitapongezwa na UN

Dkt. Samia: Kilichofanyika leo kitapongezwa na UN

Rais wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan amesema uzinduzi wa Mkakati wa Kisayansi wa Kujenga Umahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) umetekeleza lengo namba nne kwenye malengo endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDG’S).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akifurahia Mapokezi na burudani kutoka kwa Watoto wakati wa tukio la Uzinduzi wa Mpango Mkakati wa Kisayansi wa kujenga Umahiri wa Kujua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kuanzia Wanafunzi wa elimu ya Awali mpaka Darasa la Pili leo Januri 29, 2026.

Dkt Samia amesema hayo Alhamisi Januari 29,2026 akizindua Mpango Mkakati wa Kisayansi wa Kujenga Umahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa watoto wa Elimu ya Awali na Darasa la I na II.

Kwa mujibu wa Dkt Samia, lengo hilo namba nne linahimiza kuwapa watoto na vijana elimu ya hali ya juu ambayo inapatikana kwa urahisi na ina uwezekano wa ziada wa kujifunza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitembelea Mabanda na kupata maelezo ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Kisayansi wa kujenga Umahiri wa Kujua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kuanzia Wanafunzi wa elimu ya Awali mpaka Darasa la Pili eneo la Baraza la Mitihani Mwenge Dar es salaam leo Januari 29, 2026.

“Tumetekeleza mikakati yetu ndani ya Taifa, ndani ya Afrika, lakini pia kimataifa. Kwa hiyo Umoja wa Mataifa wakijua tulichokifanya leo watatupa pongezi nyingi sana, kwa haya tulioyafanya,”

“Ndugu zangu niseme, tupo katika njia sahihi na tunakwenda vizuri,” amesema Dkt Samia.

Leave a Reply