You are currently viewing Dkt Samia: Tofauti zisihatarishe amani, mshikamano wetu

Dkt Samia: Tofauti zisihatarishe amani, mshikamano wetu

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amewaambia wafanyakazi kuwa, tofauti zisigeuke kuwa sababu ya kuhatarisha misingi ya amani, umoja na mshikamo iliyoachwa na waasisi wa Taifa.

Dkt Samia ameeleza hayo leo, Ijumaa Mei Mosi,2026  wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ‘Mei Mosi’, yaliyofanyika kitaifa mkoani Njombe.

Mkuu huyo wa nchi, amejenga hoja hiyo akirejea kauli mbiu ya Mei Mosi kuwa kazi haiwezi kuwa na staha bila na amani, hakuna ustawi wa mfanyakazi bila utulivu wa Taifa.

“Tushikamamaneni, tufanye kazi, tujenge Taifa letu na tujenge heshima ya nchi yetu,” amesisitiza Dk Samia.