You are currently viewing Dkt. Samia: Waliotaka kuvuruga amani washindwe na walegee

Dkt. Samia: Waliotaka kuvuruga amani washindwe na walegee

Rais Samia Suluhu Hassan, amesema tuzo ilizotunukiwa Tanzania ikiwemo ya kuwa kituo bora cha utalii duniani ni uthibitisho wa sifa nzuri ilizonazo, huku akisema waliotaka kuivuruga amani ili kuichafua nchi, washindwe na walegee.

Tuzo ambazo Tanzania ilitunukiwa ni ile ya kituo bora cha utalii duniani, nchi bora kwa utalii Afrika, Serengeti kuwa hifadhi bora ya utalii, Zanzibar kuwa eneo la utalii wa mikutano na moja ya hoteli za Tanzania zimetunukiwa tuzo ya ubora.

Dkt Samia ametoa kauli hiyo leo, Januari 10, 2026 wakati wa hafla ya kuwapongeza wanamichezo waliofanya vizuri katika mashindano ya kimataifa Ikulu ya Dar es Salaam.

“Kwa wale waliotaka kutuharibia amani, ili kuharibu sifa ya Tanzania washindwe na walegee. Tanzania itabaki kuwa kitovu cha amani na haya tulioshinda tutaendelea kushinda miaka ya mbele inayokuja,” amesema.

Leave a Reply