BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) leo tarehe 29 Oktoba, 2024 limetangaza matokeo ya mitihani ya darasa la saba ambayo yanaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 974,229 sawa na 80.87%, watahiniwa wenye matokeo wamefaulu na kumaliza Elimu ya Msingi 2024.
Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa NECTA, Said Mohamed amesema ufaulu wa jumla umeongezeka kwa 0.29%.
Amesema kati ya watahiniwa hao wavulana ni 449,057 sawa na 81.85% na wasichana ni 525,172 sawa na 80.05%, hivyo ufaulu wa wasichana umeshuka kwa 0.53% na ufaulu wa wavulana umeongezeka kwa 1.26%.
Bofya hapa kutazama matokeo ya mtihanin wa darasa la saba. https://matokeo.necta.go.tz/results/2024/pslexj6/psle.htm