You are currently viewing Kapufi: Asilimia kubwa ya vijana nchini ni tegemezi
Sebastian Kapufi

Kapufi: Asilimia kubwa ya vijana nchini ni tegemezi

Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini, Sebastian Simon Kapufi (CCM) ametoa wito kwa Serikali kuwaangalia vijana ili wasiwe tegemezi badala yake wawe nguvu kazi ya Taifa.

Kapufi ametoa kauli hiyo leo Jumanne wakati akichangia Bungeni Jijini Dodoma Hotuba ya Bajeti Kuu la Serikali ya Ofisi ya Waziri Mkuu Tanzania.

Vijana wakibashiri (wakibeti) matokeo ya michezo mbalimbali

“Idadi ya Watanzania ni takribani milioni 60, asilimia 60 ni vijana walio chini ya umri wa miaka 25. Asilimia 32 ni vijana kati ya miaka 10 – 24. Kuwa na idadi kubwa ya watu inaweza kuwa faida au hasara, unapokuwa na idadi kubwa ambayo ni tegemezi na wachache wanaoshiriki kujenga uchumi wa nchi, tabu inaanzia hapo” amesema na kuongeza;

“Ukiwa na idadi kubwa ya watu hasa vijana na wakatumika vizuri ni msaada kwa Taifa lakini wakikutana na changamoto na wao wakawa ni tegemezi wakahitaji ajira, hilo linakuwa ni bomu.

“Mkakati wa Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana 2007 na Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana 2007, zote hizi zimesheheni namna ya kuwasaidia vijana wasiwe tegemezi”.”

Amesema Ofisi ya Waziri Mkuu inayo nafasi ya kuwasaidia vijana ikiwa ni pamoja na madirisha mbalimbali ya mikopo na fursa zingine ambazo wengine hawazifahamu huku akisisitiza kuwa wakati umefika vijana wapewe nafasi ya kutafahamu madirisha ya fursa.

“Tanzania tumeendelea kupata wadau mbalimbali waliojielekeza katika suala la uchimbaji wa Madini lakini Serikali isipokuwa makini kusimamia hili itakuta maeneo ya wachimbaji wadogo wadogo vijana wengi wamevamia bila kufuata utaratibu.

“Kupitia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI tulipita tukaona Shule za Sekondari za Wasichana za Masomo ya Sayansi, Shule hizo ni nzuri lakini kama Maabara hazitofanya kazi, tafsiri nzima ya kuitwa Shule za Sayansi inapoteza maana.

“Urejeshaji wa Miundombinu iliyoharibika kama miradi ya dharura, Mpanda Mjini kuna maeneo yana miradi mikubwa ya Umwagiliaji ya takribani shilingi Bilioni 31, maeneo haya kama Miundombinu imeharibika yasipoweza kufikiwa hata tafsiri ya mradi inapoteza maan,” amesema.

Leave a Reply