Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KATIKA kuunga mkono dhamira ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda yakuendeleza michezo yote nchini kwa vitendo, Shule yakimataifa ya Monti International School imetangazakuandaa tukio kubwa la kipekee la michezo kwa ukandawa Afrika Mashariki — kambi maalum ya kuogelea yasiku 10 itakayoongozwa na kocha maarufu kutokaMarekani, Austin Pillado.
Kambi hiyo ya kiwango cha juu (High-Performance Swim Camp) inatarajiwa kufanyika kuanzia Mei 5 hadiMei 14, 2026 katika kampasi ya Mikocheni, jijini Dar es Salaam.
Kocha Pillado, ambaye ni Naibu Kocha Mkuu wa timu yawanawake ya kuogelea kutoka Chuo Washington State, pia alikuwa sehemu ya benchi la ufundi lililoshindaubingwa wa mashindano ya juu kabisa ya michezo yavyuo vikuu nchini Marekani, yanayoandaliwa na National Collegiate Athletic Association (NCAA) mwaka 2024 akiwa na Arizona State University.
Akiwa na uzoefu wa kufanya kazi na mabingwa waOlimpiki na washikiliaji wa rekodi za dunia, ujio wake unatajwa kuwa hatua muhimu kwa maendeleo ya michezoya vijana nchini.
Akizungumza kuhusu tukio hilo, Mkurugenzi mkuu naMwanzilishi wa shule hiyo, Fatma Fernandes alisemalengo kuu ni kuinua viwango vya vipaji vya ndani kufikiahadhi ya kimataifa.
“Tunataka kuziba pengo kati ya vipaji vya ndani naviwango vya kimataifa. Kwa kuwaleta makocha wakiwango cha juu kama Austin, tunawezesha vijana wetukupata mafunzo na uchambuzi wa kitaalamu sawa nawanariadha bora duniani,” alisema Fernandes.
Kambi hiyo itakuwa ya kwanza katika ukanda huukutumia teknolojia ya kamera za chini ya maji(underwater cameras) inayotoa mrejesho wa papo kwapapo kuhusu mbinu za waogeleaji. Mbali na mazoezi yakimwili, washiriki watapata mafunzo ya ziada kuhusumikakati ya mashindano, lishe bora na mbinu ya “Fifth Stroke” inayohusisha mbinu za uogejeleaji ambazo nimuhimu katika ushindani wa kisasa.
Kwa mujibu wa waandaaji, programu hiyo imeundwakwa kuzingatia mitaala ya vyuo vikuu vya Marekanivinavyoshiriki mashindano ya NCAA, ikilengakuimarisha stadi za mbinu nne kuu za kuogelea pamoja nakuendeleza uwezo wa uvumilivu na kasi.
Uongozi wa Monti umeeleza kuwa uwekezaji katikamiundombinu ya michezo, ikiwemo bwawa la kisasa la mita 25 la kiwango cha Olimpiki, una lengo la kunufaishasi wanafunzi wa shule hiyo pekee bali pia jamii pana yaDar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.
Kambi hiyo pia inatarajiwa kuvutia washiriki kutoka nchijirani za Afrika Mashariki, huku nafasi zikitajwa kuwachache ili kuruhusu ufuatiliaji wa karibu wa maendeleo yakila mshiriki.
Hatua hiyo inaonekana kuwa mchango mkubwa katikakuiweka Tanzania kwenye ramani ya kimataifa ya mchezowa kuogelea, huku ikienda sambamba na malengo yaBaraza la Michezo nchini (BMT) ya kuendeleza, kuratibu, na kudhibiti michezo ili kuinua vipaji na ushindani.
