You are currently viewing Kutoka Kampala hadi Kizimkazi, Jose Chameleone akitoa burudani

Kutoka Kampala hadi Kizimkazi, Jose Chameleone akitoa burudani

Mwanamuziki kutoka Uganda, Joseph Mayanja maarufu kama Jose Chameleone, ni miongoni mwa wasanii wanaotoa burudani katika Tamasha la Kizimkazi 2026, hatua inayoonesha namna tamasha hilo linavyozidi kuvuka mipaka ya Tanzania na kuvutia washiriki kutoka Afrika Mashariki na maeneo mengine ya Afrika.

Chameleone alitumbuiza katika Usiku wa Kizimkazi na leo ametoa burudani katika hafla ya kilele cha tamasha hilo mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Tamasha la Kizimkazi 2026, lenye kaulimbiu “Kizimkazi Kumenoga: Shangwe na Fursa,” lilianza Agosti 12 na linafikia kilele leo, Agosti 14, katika Uwanja wa Mwehe, Makunduchi.

Xxxxxx

Dk Mwinyi: Tamasha la Kizimkazi ni chachu ya utalii na uwekezaji

Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, amesema Tamasha la Kizimkazi linapaswa kuendelea kuwa chachu ya kuvutia wageni Zanzibar na kuhamasisha utalii wa ndani pamoja na shughuli za uwekezaji.

Akizungumza leo, Agosti 14, 2026, katika kilele cha Tamasha la Kizimkazi kinachofanyika Uwanja wa Mwehe, Makunduchi, Dk. Mwinyi amesema tamasha hilo lina nafasi muhimu katika kukuza utalii na uwekezaji, si Zanzibar pekee bali pia Tanzania kwa ujumla.

“Ni matumaini yangu kuwa Tamasha hili la Kizimkazi litaendelea kuwa chachu na kutoa mchango muhimu wa kuwavutia wageni hapa Zanzibar na kuhamasisha utalii wa ndani na shughuli za uwekezaji hapa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla,” amesema Dk. Mwinyi.