Na Mwandishi Wetu
Maelfu ya wafuasi wanayoiunga mkono serikali ya Venezuela wameandamana katikati mwa mji mkuu Caracas wakitaka kurejeshwa rais aliyeondolewa madarakani Nicolás Maduro na mke wake Cilia Flores.
Maelfu ya wafuasi wanayoiunga mkono serikali ya Venezuela wameandamana katikati mwa mji mkuu Caracas jana Jumanne, wakitaka kurejeshwa rais aliyeondolewa madarakani Nicolás Maduro na mke wake Cilia Flores ambao sasa wanazuiliwa na mamlaka za Marekani.
Waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo Diosdado Cabello, mmoja wa wanasiasa wenye ushawishi mkubwa nchini humo, alijiunga na waandamanaji waliokuwa wamebeba mabango, picha za Maduro na bendera za taifa huku wakiimba nyimbo za kumuunga mkono Maduro na Flores.
Cabello aliwahutubia waandamanaji hao na kuwataka waendelee kusimama kidete na kutoa mwito kwa Marekani kuwaachilia wawili hao.
Amesema hatua ya kuwakamata Maduro na mkewe ni “jaribio la kudhoofisha uhuru wa Venezuela” na amesisitiza kuwa wananchi “hawatakubali kuona taifa lao likidhalilishwa.”
Maandamano hayo yamefanyika siku moja baada ya Makamu wa Rais wa Venezuela, Delcy Rodríguez, kuapishwa kuwa Rais wa mpito.
