You are currently viewing Maofisa bajeti Magu wapewa mafunzo ya uandaaji, utekelezaji wa mipango na bajeti

Maofisa bajeti Magu wapewa mafunzo ya uandaaji, utekelezaji wa mipango na bajeti

Halmashauri ya Wilaya ya Magu leo Alhamisi tarehe 27 Novemba 2025 imetoa mafunzo ya uandaaji na utekelezaji wa mipango na bajeti kwa maafisa bajeti wa idara na vitengo pamoja na watumishi wa idara ya afya.

Mafunzo hayo yanalenga kuwaongezea ufanisi na uelewa katika kipindi cha uandaaji wa mipango na bajeti katika maeneo yao ya utendaji kazi, ili kuhakikisha mipango yao inaendana na bajeti wanazoziweka.

Hatua hiyo ni maandalizi ya kuelekea uandaaji wa mipango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu, Mohamed Ramadhani, Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu, Mophen Mwakajonga amewataka wataalaam hao kuhakikisha wanazingatia mafunzo hayo ili kuweza kuwa na bajeti bora.

Katika mafunzo hayo yaliyotolewa na wakufunzi Lameck Kurwa na Beatrice Mdanku kutoka divisheni ya mipango na uratibu ya halmashauri ya wilaya ya Magu, washiriki wamefundwa namna ya kuingiza mipango na bajeti kwenye mfumo unaohusika na uandaaji wa bajeti (PLANREP).

Leave a Reply