You are currently viewing Mbarawa: NIT zalisheni marubani watakaotumia ndege mafunzo kwa ufanisi

Mbarawa: NIT zalisheni marubani watakaotumia ndege mafunzo kwa ufanisi

Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, ameutaka uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kuhakikisha kinazalisha marubani wa kutosha ili kuongeza ufanisi katika matumizi ya ndege mbili za mafunzo ya urubani zilizopo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Akizungumza leo, Oktoba 17, 2024, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Pili la Kimataifa katika Uchukuzi na Usafirishaji lililofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, Prof. Mbarawa alibainisha kuwa NIT imezalisha marubani nane pekee mwaka huu, badala ya marubani 10 waliotarajiwa.

Aidha, Prof. Mbarawa aliongeza kuwa ongezeko la marubani litasaidia kukidhi mahitaji ya mashirika ya ndege kama Air Tanzania, ambayo kwa sasa yana uhitaji mkubwa wa marubani.

Kongamano hili ni la pili kufanyika, baada ya kongamano la kwanza kufanyika Oktoba 19, 2023. Lengo kuu la makongamano haya yanayoandaliwa na NIT ni kujadili fursa na changamoto mbalimbali katika sekta ya uchukuzi. Kongamano la mwaka huu limeanza rasmi leo na linatarajiwa kufungwa Oktoba 19, 2024.

Leave a Reply