Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema tangu kuanza kwa safari ya treni ya kisasa inayotumia umeme (SGR) katika mikoanya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma, tayari imekusanya kiasi cha Sh bilioni 15.69.
Amefafanua kuwa Shirika la Reli Tanzania (TRC) limefanikiwa kukusanya kiasi hicho cha mapato kuanzia tarehe 14 Juni mwaka huu treni hiyo ya kisasa ilipoanza kutoa huduma hadi kufikia tarehe 3 Septemba 2024,
Prof. Mbarawa amesema kwa kipindi hicho, SGR imesafirisha abiria 645,421 katika safari zake za kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro na Dar es Salaam kwenda Dodoma.